Waziri wa Uchukuzi,Mh. Omari Nundu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na utendaji kazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Siku za hivi karibuni utendaji kazi wa TAZARA umekuwa wa kusuasua kutokana na matatizo mbalimbali yanayolikabili Shirika hilo.
Baadhi ya viongozi wa Umoja wa Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) tawi la TAZARA wakijadili mambo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa utendaji kazi wa Mamlaka ya TAZARA baina ya Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Siku za hivi karibuni utendaji kazi wa Mamlaka hiyo umekuwa wa kusuasua kutokana na matatizo mbalimbali yanayolikabili Shirika hilo.Kutoka kulia ni Lufingo Mwanghba, Bundala Kabulwa, Yassin Mleke na Benjamini Kehogo.
Baadhi ya watendaji wakuu wa wizara ya Uchukuzi wakimsikiliza Waziri Omari Nundu (hayupo pichani) wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na utendaji kazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) leo jijini Dar es Salaam. Siku za hivi karibuni utendaji kazi wa TAZARA umekuwa wa kusuasua kutokana na matatizo mbalimbali yanayolikabili Shirika hilo. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhandisi Omari Chambo.Picha na Anna Nkinda - Maelezo
No comments:
Post a Comment