Wednesday, March 21, 2012

SBL YAZINDUA MRADI WA KUVUNA MAJI YA MVUA IRINGA


Pichani kati ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge akizindua mradi wa kuvuna maji ya mvua mapema leo katika hospitali ya Frelimo ya Manispaa ya Iringa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maji duniani itakayoadhimishwa tarehe 22 Machi 2012,Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano (SBL),Bi Teddy Mapunda  na kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa,Bi.Theresia Mhongwe wakishishuhudia tukio hilo .Mradi huo umefadhiriwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia mradi wake wa EABL Foundation

========  ========  ===== =====.
SBL YAZINDUA MRADI WA KUVUNA MAJI YA MVUA IRINGA.
Mradi huo kuwezesha  zaidi ya watu 150,000 kupata maji safi na salama

Machi 21, 2012
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia mradi wake wa EABL Foundation leo imezindua mradi wa uvunaji maji katika hospitali ya Frelimo ya Manispaa ya Iringa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maji duniani itakayoadhimishwa tarehe 22 Machi 2012.

Zaidi ya watu wapatao 150,0000 wanaohudumiwa na hospitali hiyo watanufaika. Maadhimisho ya wiki ya maji nchini Tanzania yafanyika kitaifa mjini Iringa. 

Mradi huu wa uvunaji wa maji ya mvua ulifikiwa baada ya kushauriana na Wizara ya maji na Manispaa na kutambua wingi wa maji yanayopotea ambayo yangeweza kuvunwa kwa matumizi.

Mradi unatarajiwa kutumia kiasi cha zaidi yashilingi  milioni 50 ikiwa ni gharama za ununuaji na uwekaji wa matanki ya maji, mabomba, pampu ya umeme na ukarabati mdogo wa miundo mbinu iliyopo.

Kampuni ya bia ya Serengeti inafahamu na inatambua umuhimu wa maji duniani na hata katika biashara yetu, na ndio maana basi tunashiriki kikamilifu katika kuhamasisha upatikanaji wa maji safi na salama.

Kwa mwaka huu pekee Kampuni ya Bia ya Serengeti imetenga zaidi ya shilingi milioni 300 katika miradi ya maji.Kati ya hizo, shilingi milioni 100 ni kwa ajili ya udhamini wa wiki ya maji ambazo zimetumika katika matangazo , mabango ya matangazo , fulana, kofia , vipeperushi , vijarida n.k. 

Kiasi kilichobaki cha shilingi milioni 200 ni kwa ajili ya miradi endelevu ya maji katika mikoa ya Iringa , Mwanza, Moshi na Dar es Salaam.

Kama kampuni inayowajika ,tumekuwa tukijihusisha na miradi mbalimbali ya maji safi na salama ukiwemo ule Mkuranga. Na pia tumeshiriki katika mradi wa kuboresha maji katika Hospitali Amana kwa kushirikiana na makampuni mengine na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Katika mradi wa Mkuranga , Kampuni ya Bia ya  Serengeti imewekeza zaidi ya shilingi milioni 384.6 ambapo zaidi ya watu 250,000 wananufaika na mradi huu.

Kampuni ya Bia ya Serengeti itaendelea kufadhili miradi endelevu ya kuisadia jamii hasa miradi ya maji, ili kwa pamoja tuweze kupunguza na kuboresha miundombinu na upatikanaji wa maji safi na salama.

No comments:

Post a Comment