Thursday, March 22, 2012

hoja ya haja: tuhuma za ulevi dhidi ya vijana wa shule

Assalam  Alaikum Kaka.
 kwa muda sasa vilio vya wazazi na waalimu vimekuwa vikisikika kuhusiana na tuhuma za vijana wa shule kujihusisha na matumizi ya vileo.mimi ni mwalimu katika shule moja mkoa wa kielimu Temeke,DSM.

Nimepigania kupinga  hili jambo la kukodisha wafanya biashara wa kuuza vileo katika shule yangu hadi nikaonekana ninaajenda yangu ya siri.Ukweli nakwamba ninaandika roho inaauma kuona baadhi ya waalimu hawana uchungu na maisha ya watoto amabao sisi tumepewa jukumu la kuwalea kwa kipindi cha miaka saba (7).

Baadhi ya waalimu wamekuwa wakifaidika na vijisenti vya upangishaji na mikataba ambayo mwisho wa siku inaharibu mwelekeo wa watoo wetu.

Hebu UNCLE wewe na timu yako kwa muda wenu njoo hapa shuleni  (kurasini primary karibu na UHAMIAJI HQ) uone duka la vilevi tena vikali waliyopewa dhamana ya kuharibu wanafunzi na uongozi wa shule.
naomba ufiche jina langu 
nisiharibu salary slip yangu.asante
Ticha 

No comments:

Post a Comment