Monday, March 19, 2012

msaada tutani: mdau mariam aomba msaada kusaidia yatima anaowatunza

 Mimi naitwa Miriam, 
Ninawatunza watoto  watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 30 .Watoto hawa wana umri  kati ya miaka 4-13. Nimefanikiwa kufungua kituo cha watoto maeneo ya Mbezi Mwisho ambapo watoto 10 (wa kike) wanakaa hapo kwa sasa kwani hawakuwa na mahali pa kukaa kabisa. 


Nimeshindwa kuwaweka wote kwenye kituo kwa sababu sina pesa ya kuwahudumia wote kwa wakati mmoja wakiwa hapo kituoni na mimi lengo langu ni kuwasaidia waweze kupata maisha bora.


Pamoja na kufanikiwa kufungua kituo nina changamoto za mahitaji kama vitanda, magodoro hayatoshi, sare za shule za watoto, mashuka,chakula, simtank la maji,nguo za watoto, meza na viti vya kusomea na mahitaji mengine madogomadogo. Pia tunaomba kama kuna mtu ataguswa kutusaidia fridge ili tuweze kuhifadhi  chakula na vitu vingine kwa wingi ili kupunguza gharama ya kununua vitu kila siku.

Kwayeyote atakayeguswa kutusaidia wasiliana nasi kwa  namba 
+255757 855 858 au +255655 855 858
 Watoto wanaolelewa kituoni hapo

No comments:

Post a Comment