Tuesday, March 20, 2012

AICC YAPATA TIMU KATIKA MICHUANO YA MEI MOSI MWAKA HUU

Wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kutoka kushoto-Saumu Kilari, Elizabeth Amandus, Evalyna Kunkuta na Zainab Ramadhan, wakijiandaa kuanza mbio za baiskeli katika mashindano yaliyoandaliwa na kituo hicho katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mwishoni mwa wiki jijini Arusha, kutafuta wawakilishi watakaoenda Tanga katika mashindano ya Mei Mosi. Katika mbio hizo Elizabeth Amandus aliibuka mshindi.
Wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Eva Kunkuta (kulia) na Latifah Amiri wakichuana katika mchezo wa Draft uliofanyika mwishoni mwa wiki katika mashinda ya kutafuta wachezaji watakao iwakilisha AICC katika mashindano ya Mei Mosi jijini Tanga.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa AICC, Savo Mung’ong’o (kushoto) akisukuma kete dhidi ya Leonard Ngasa katika mchezo wa Draft uliofanyika mwishoni mwa wiki Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutafuta wawakilishi watakaoenda Tanga katika mashindano ya Mei Mosi.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Savo Mung’ong’o (wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho na waamuzi baada ya kumalizika kwa mashindano ya kutafuta wachezaji watakao wakilisha kituo hicho katika mashindano ya Mei Mosi jijini Tanga. Mashindano hayo ya mchujo yalifanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kimechagua wachezi timu ya wachezaji kumi itakayo wakilisha kituo hicho katika mashindano ya kuadhimisha sherehe za Mei Mosi mwaka huu zitakazo fanyika kitaifa jijini Tanga.

Wachezaji hao walichaguliwa baada ya kituo hicho kufanya mashindano ya mchujo mwishoni mwa wiki kupata wawakili watakaoenda Tanga katika mashindano hayo yatakayoanza katikati ya mwezi wa nne.

Mashindano hayo ya mchujo yalishikisha mchezo wa mbio za baiskeli kwa wanaume mita 4000 na mita 2000 kwa wanawake, riadha mita 1200 kwa wanaume na wanawake mita 800, drafti kwa wanaume na wanawake, bao wanaume na wanawake na karata wanaume na wanmawake.

Katika mbio za baiskeli wanaume, Boniface Rutunda aliibuka mshindi akifuatiwa na Rodney Thadeus na nafasi ya tatu ilishikwa na Proches Kamugisha. Wakati wanawake Elizabeth Amandus alinyakua ushindi wa kwanza akiwaacha Saumu Kilari na Zainabu Ramadhan walioshika nafasi ya pili na tatu.

Kwa upande wa riadha, Fidel Kweka aliongoza na kuwaacha John Martin aliyeshika nafasi ya pili na Hiza alishika nafasi ya tatu wakati Zamda Mfaume aliibuka kidedea akifuatiwa na Redempta Shirima aliyeshika nafasi ya pili.

Kwa upande wa mchezo wa draft kwa wanaume, Rashid Rashid aliibuka mashinda baada ya kumshinda Leonard Ngasa katika hatua ya fainali, huku Eva Kunkuta akiibuka bingwa kwa upande wa wanawake baada ya kufunga Teddy Mapunda.

Katika mchezo wa karata, John Martin akiibuka mshindi katika mchezo wa Karata baada ya kumshinda Proches Kamugisha na kwa upande wa wanawake June Masubo aliibuka mshindi.

Meneja wa timu za AICC, Rodney Thadeus amesema kuwa washindi waliopatikana wanaandaliwa programu ya mazoezi ili kuhakikisha wanapata ushindi katika mashindano hayo yatakayofanyika jijini Tanga.

Nae Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa AICC, Savo Mung’ong’o amesema AICC itaendelea kuhamasisha wafanyakazi wake kushirii michezo mbalimbali na kwamba shiriki linaandaa utaratibu wa kufanya mazoezi kila wiki.

No comments:

Post a Comment