Monday, March 19, 2012

TBL YATOA MILIONI 25 kwa UCHIMBAJI VISIMA VYA MAJI geita

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Geita, Daud Sweka kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo za kusaidia mradi wa visima vitatu  vya maji safi na salama ya kunywa kwa wakazi wa Kijiji cha Mkolani-1 wilayani humo hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mauzo wa TBL Geita, Issa Msuya. 
Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamakale, Sizya Mulelemi Mashilungu akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 25 Enock Kangasa, mkandarasi anayatekeleza mradi wa visima vya maji safi na salama ya kunywa kwa ajili ya wananchi wa  kijiji cha Mkolani-1 Geita Mwanza, muda mfupi baada ya hundi hiyo kutolewa na kampuni ya Bia nchini (TBL). Kulia anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa TBL Editha Mushi. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBl), Editha Mushi (mwenye miwani) akipata maelezo  kutoka kwa mkandarasi, Enock Kangasa (mwenye shati jeupe la mikono mifupi ) ambaye anachimba visima vya maji  katika Kijiji cha Mkolani, Geita, kuhusu 'ring' zinazotumika katika ujenzi wa mradi wa visima vya maji uliofadhiliwa na  kampuni ya TBL  kwa sh. milioni 25. Hafla ya kukabidhi hundi ilifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki. (NA MPIGAPICHA WETU)

Baadhi ya wananchi wa Nyamakale Mkolani -1  wakiwa na hundi ya sh. milioni 25 walizopewa na TBL 

No comments:

Post a Comment