Tuesday, March 20, 2012

NAIBU SPIKA ATEULIWA MWENYEKITI WA KIKAO CHA PAMOJA CHA MABUNGE YA AFRIKA,CARIBBEAN NA PACIFIC

 Mhe. Job Ndugai, Mb na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akijiandaa kuongoza kikao cha pamoja cha wabunge toka nchi za Afrika, Caribbean na Pacific kinachofanyika jijini Brussels kuanzia jana. Katika kikao hicho Mhe. Naibu Spika alianza rasmi nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Jamii na Mazingira ambayo ataishikilia kwa miaka miwili ijayo. Mhe. Naibu Spika ataongoza kamati hiyo iliyoko kwenye jumuiya ya nchi za Afrika, Caribbean na Pacific ambayo ina jumla ya nchi wanachama 79. Wa pili kulia ni Mbunge toka Tanzania, Mhe. Dr. Mary Mwanjelwa ambae pia anashiriki mkutano huo.
Mhe. Naibu Spika akiwa na balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji aliemaliza muda wake, Mhe. Balozi Mlay (katikati) katika picha ya pamoja na Afisa wa Ubalozi huo Bw. Cheche mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Kamati ya Masuala ya Jamii na Mazingira.Picha na Saidi Yakubu,Brussels.

No comments:

Post a Comment