Monday, March 19, 2012

bonanza la kitambi noma lazidi kushamiri jijini arusha


Jana jumapili ya tarehe 18/03/2012 kwenye viwanja vya KIITEC kulikuwa na muendelezo wa Bonanza la kila jumapili KITAMBI NOMA BONANZA kulikuwa na michuano ya soka pamoja na uvutaji wa kambi (Tag of War) ambapo matokeo kwa upande wa soka yalikuwa kama ifuatavyo:

KITAMBI NOMA 5 - 1 ARUSHA STARS (Nyota wa mchezo - Ramadhani Kabadi)
KITAMBI NOMA 3 - 2 ACCESS FC (Nyota wa mchezo - Sam Msukuma)
ARUSHA STARS 2 - 4 ACCESS FC (Nyota wa mchezo - Mike Access)

Na kwa upande wa mashindano ya kuvuta kamba timu ya wanawake ya KITAMBI NOMA QUEENS iliibuka washindi kwa kuivuta timu ya wanawake ya ARUSHA STARS mara nne katika raundi tano dhidi ya raundi moja ya Arusha Stars.

Mbali na michezo hiyo kuchukua nafasi pia kulikuwapo upinzani mkubwa wa kutoa burudani baina ya ACCESS FC na KITAMBI NOMA ktk viunga vya QX PUB, huku ACCESS FC wakichukua point 3 tatu muhimu baina ya kutoa burudani ya kufa mtu pale QX PUB ikiwaacha wanaKITAMBI NOMA CLUB wasiamini kilichotokea kilabuni kwao.

Kufuatia kushindwa kutoa burudani, Mwenyekiti Nd. Chalz Makwaia wa KITAMBI NOMA alijitetea kuwa vijana wake siku ya jana walikuwa katika mchakato mzito wa kupata ripoti ya mapato na matumizi ya kilabu hivyo wakashindwa kutoa 'kwachu-kwachu' kama kawaida yao

No comments:

Post a Comment