Tuesday, March 20, 2012

Kamera ya Globu ya Jamii na matukio mbali mbali mji kasoro bahari leo

Mama aliekuwa na watoto wake wawili,Mmoja akiwa amembeba mgongoni na mwingine akiwa amemshika mkono huku akiwa na mzigo kichwani na mwingine mkononi akielekea nyumbani wakati akitokea mahala anakofanya shughuli zake kama alivyonaswa na Kamera Man wa Globu ya Jamii leo,Mkoani Morogoro.
Watoto ambao umri wao ni wa kuwa shuleni hivi sasa,wakifanya biashara ya kuuza ndizi pembezoni kwa barabara ielekeayo Morogoro Mjini.
Wakazi wa Mji wa Morogoro wakitoka sokoni kununua bidhaa mbali mbali.
Mkaa ukipelekwa sokoni.
Abirira wa Basi la Champion lifanyalo safari zake kati ya Dar-Dodoma wakiwa wamesimama huku wakitafakali la kufanya mara baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kuharibika wakati likiwa safarini,mapema leo asubuhi nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Wanafunzi wakitoka kuteka maji mali na shule wasomayo kwa ajili ya matumizi mbali mbali shuleni kwao.
Safari ni hatua na kina Mama hawa wanalidhihirisha hilo.

No comments:

Post a Comment