Tuesday, March 20, 2012

SHIRIKISHO LA WANACCM VYUO DSM

                                                                      TAARIFA.
 
1.TUNATOA PONGEZI ZETU ZA DHATI KWA RAIS KIKWETE NA MADAKTAR KWA KITENDO CHAO CHA KIZALENDO CHA KUMALIZA MGOMO WA MADAKTARI,tunaomba hekima hiyo iwe inatumika mapema kwa pande zote ili kuiepusha jamii na majanga.
 
2.Tunatumia nafasi hii pia kuitaka bodi ya mikopo na wizara ya elimu kutoa ufafanuzi juu ya marakebisho yatakayofanyika kwa bodi ya mikopo baada ya kutoa maoni yetu katika tume ya maboresho ili kupunguza usumbufu wa bodi kwa maadhi ya vyuo na wanafunzi, ambao hupo mpaka sasa.Wezi wa fedha za bodi tunaomba mahakama ifanye kazi yake kwakuwatolea mfano wachakachuaji wanaohusika.Tunaamini vyuo vya Dar es salaam bila migomo inawezekana.
 
 
3.Tunaiomba serikali kusikiliza kilio cha muda mrefu cha wanafunzi wa chuo cha kumbukumbu ya mwalimu nyerere juu ya gharama kubwa za matibabu ya laki moja kila mwaka ambapo ata wenye bima za afya utakiwa kulipa gharama hizo kwa wakati mmoja, mwanachuo aumwe asiumwe utakiwa kulipa gharama hizo kila mwaka na kwamujibu ya kanuni za chuo (prospectos na by laws) gharama hizo ni kwa zahanati ya chuo tu ambapo mwanachuo hapewi kitambulisho chochote kama bima ya matibabu na akiwa likizo bado ugharamika gharama nyingine za matibabu.
 
4.Tunaiomba serikali na uongozi wa vyuo husika kuwasamehe wanavyuo wenzetu waliofukuzwa vyuo au kusimamishwa ambao wamekiri makosa yao,mfano wanachuo wenzetu 33 wa chuo cha afya muhimbili, wa mwaka wanne na wa tano ambao wamesomeshwa kwa pesa za umma na ambao walikiri makosa yao mbele ya jamii na kwa uongozi wa chuo,tunaomba madaktari hawa wanafunzi wasamehewe kwani mpaka sasa hawajui mustakibali wao,tunaamini lilipofikia swala hili serikali yetu sikivu haitakata mkono kisa umewekwa kinyesi na mtoto.Tunaomba pia wa nachuo wenzetu kuwa makini vyuoni nakutotumika na watu ambao migomo vyuoni huwanufaisha,na inapotokea wanachuo kufukuzwa huwakimbia.
 
5.Tunaiomba serikali kuangalia utaratibu wa kuwapa nafaka kama mchele/mahindi/maharage toka maghala ya taifa kwa bei nafuu wazabuni wa vyakula vyuoni ilikupunguza gharama za chakula vyuoni ambapo kwa baadhi ya vyuo nikubwa sana.
 
6.Serikali pia ingalie utaratibu wa ujenzi wa hosteli za pamoja kwa mfano tunashauri ujenzi wa hosteli eneo la kigamboni utasaidia sana wanavyuo wa vyuo vya kati ya mji ambao makazi kwao imekuwa shida na ukizingatia nyumba za jangwani zilikumbwa na mafuriko,wanafunzi wa IFM,MNMA,CBE,IAE, bado hupanga mitaani ambapo gharama ni kubwa sana na sasa chumba hufikia shilingi elfu sabini mpaka laki moja kwa maeneo ya kigamboni ambayo wanafunzi wengi wa IFM,CBE,na MNMA hupanga.
 
TUNAIMANI KUBWA NA SERIKALI YA CCM KUWA INASIKIA NA INATENDA.
 

No comments:

Post a Comment