Thursday, March 22, 2012

MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI JAJI MSATAAFU JUBUVA AONGELEA UCHAGUZI WA JIMBO DOGO LA ARUMERU MASHARIKI

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Msataafu Damian Lubuva(katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo  Ukumbi wa mkutano wa Ofisi ya Tume ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali ya Uchaguzi  Mdogo unaotegemea kufanyika April 1,2012  Jimbo la Arumeru Mashariki  ambalo amesema  litatumika daftari liliotumika  katika Uchaguzi wa mwaka 2010.ambalo limefanyiwa marekebisho na kutumika ktika Uchaguzi mdogo utakaowashirikisha jumla ya wapiga kura 127,455.Awali daftari la wapiga kura liliotumika katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 lilikuwa na wapigakura 127,429. na baada ya marekebisho litakuwa na nyongeza ya wapiga kura 26  Makamu Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Msataafu wa Zanzibar Mh Hamid Mahmoud Hamid na kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Mallaba,  (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO). 

No comments:

Post a Comment