Asalaam Aleyikum Ankal Issa Michuzi.
Ninaitwa Wilbald. Ankal nina jambo ambalo naomba unisaidie kuliweka katika blog yako ili Watanzania wenzangu waelewe. Mnamo tarehe 25/01/2012 Indian High Commission Office ilitoa tangazo la Indian scholarships katika fani mbalimbali kwa Watanzania katika gazeti la Kiingereza la Daily News kwa vyuo mbalimbali vya India.
Tarehe ya mwisho wa kutuma maombi kwa mujibu wa hilo tangazo ilikua ni tarehe 20/02/2012, candidates walishauriwa kupiga simu Indian high Commission kati ya tarehe 07 na 08 March kuulizia status ya maombi yao. Kwenye tangazo zilitolewa namba za simu kwa ajili ya waombaji kupiga simu kwa tarehe tajwa kuulizia majibu ya maombi yao.
Nilituma maombi yangu tarehe kabla ya tarehe ya mwisho ya kutuma maombi. Ilipofika tarehe 07/03/2012, siku ambayo kwa mujibu wa tangazo waombaji walitakiwa kufuatilia majibu ya maombi yao, nilipiga simu ubalozi wa India kuulizia majibu ya maombi yangu.
Mtu niliyezungumza nae (Jina namuhifadhi)aliniambia kwamba majina ya waliochaguliwa yapo getini pale ofisi za ubalozi wa India hivyo kama ninaweza niende kuangalia. Nikaenda kuangalia, kweli nilipofika pale ubalozi wa India, nilikuta list ya majina kama 59 kwa mlinzi wa getini. Kwa bahati nzuri jina langu lilikuwepo katika waombaji waliochaguliwa.
Mlinzi akanielekeza niende kumwona ofisa anayeshughulika na mambo ya elimu (Jina namuhifadhi kwa sasa) kwa maelekezo zaidi. Nilipofika mapokezi nilizungumza na ofisa elimu wa Indian High Commission kwa simu na kunipa maelezo kwamba nirudi saa nane mchana kwa vile mda huo alikua na kazi ya kukusanya fomu za waombaji ambao tayari wameshazirejesha. hivyo akaniambia nije kuchukua fomu yangu saa nane mchana.
Kama nilivyoelekezwa nilirudi saa nane mchana. Mlinzi akampigia tena simu yule ofisa wa elimu kumjulisha kwamba nimerudi. Mlinzi akanipatia simu nizungumze na yule ofisa wa elimu. Yule Ofisa wa Elimu akanieleza kwamba samahani sana watu waliorejesha fomu wameshatosha hakuna tena nafasi.
Nilifadhaika sana. Kuna waombaji wengine walifika mda huo wa mchana kuja kuangalia majina, kwani walipopiga simu waliambiwa majina yapo getini. Cha ajabu mda ule walipofika ile list ya waombaji waliochaguliwa ilikua imekwishaondolewa pale kwa mlinzi. Na kila aliyeulizia aliambiwa tu hajachaguliwa kwani waombaji waliochaguliwa wameshapigiwa simu. Walipouliza kuhusu list waliambiwa listi imechukuliwa na Mheshimiwa Balozi.
Sasa najiuliza kama waombaji tayari wameshapigiwa simu, walipigiwa lini? kwani tangazo lilisema waombaji wapige simu kati ya tarehe 07 na 08 March 2012. Zaidi ya hapo nilimtumia barua pepe huyu ofisa wa elimu tarehe 06/032012 kuulizia majibu ya maombi yangu lakini sikujibiwa.
Hiyo ndio hali halisi Ankal Michuzi, nimeshakata tamaa na ninaomba uma wa Watanzania ujulishwe namna hizi scholarships zinavyoendeshwa. Niliomba kufanya appointment na Balozi nimweleze yaliyojiri, sikupewa nafasi na wala sikujibiwa lolote la maana.
Nakutakia kazi njema Ankal Issa Michuzi
No comments:
Post a Comment