Saturday, March 3, 2012

ASKARI MAGEREZA MLEVI?

 Uncle Mithupu habari yako bwana.
naomba utoe habari hii watanzania waone jinsi vyombo vyetu vya usalama vinavyotumia vibaya magari na vifaa vya kazi wanavyopewa vilivyonunuliwa kwa kodi zetu.Hiyo gari yenye plate number STK leo mchana mida ya saa saba kasoro imenigonga kwa nyuma nikiwa na gari yangu aina ya Toyota Carina ti nikiwa nafika hapo Gold star ofice ndogo za tigo.Huyo askari magereza aliekuwa anaendesha gari hilo alikuwa spidi mbaya akiwa anakata kona ya co-cabs akakutana foleni ghafla akanigonga nyuma kwa nguvu nikaenda kuigonga gari ya mbele yangu kama unavyoona hizo picha hapo.Askari huyo akataka kukimbia nikamzuia hapo na kmuita trafiki apime.Reaport iliyoandikwa hapo nilitamani nilie maana imeingizwa siasa na kuonekana jamaa hana makosa eti trafick anaandika reaport twende mahakamani.Nikaona hapa hizi siasa nimeshagongwa bado nikapigishwe kwata la kwenda mahamani na gari ikapaki centro kunguru wainyee pale iendelee kuoza? na bado reaport imeshachakachuliwa,Bosi wangu nampa taarifa anaona nadaiveji nimeenda kwenye ishu zangu sasa na huko mahakani ntaenda jumapili isiyo siku ya kazi?.nikaamua nikokote kamkokoteni kangu niondoke, Hapa ankal na deni la kumlipa jamaa wa mbele + nirekebishe kisoteo changu kweli nchi hii bado hatuja pata uhuru.
Mbeba box wa dar.
 KBUUUUMMMM.....
inabidi nikaripee hasara hii

No comments:

Post a Comment