Monday, March 19, 2012

Wanafunzi wa shule ya sekondari St Benedictine wafanya mdahalo wa kujiepusha na ukimwi

Kaimu mkurugenzi wa halmshauri ya wilaya Namtumbo Constatino Mushi kushoto akimfariji mwanafunzi wa kidato cha 3 shule ya sekondari Runa wilayani humo Abdul Ngonyani aliyevunjika mkono wake wa kulia kufuatia gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na wengine kujeruhiwa,katika ni baba mzazi Abdul Mang'inyuka,
Mwezeshaji wa mafunzo ya ukimwi kutoka idara ya maendeleo ya jamii ya halmshauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Pees Kamugisha akitoa mada wakati wa mdahalo wa wazi juu ya maambukizi mapya ya ukimwi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari  st benedictine hanga, uliofanyika jana shuleni hapo,
Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi ya halmshauri ya wilaya ya namtumbo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmshauri hiyo Kassim Ntara akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya St Benedictine Hanga wakatri wa mdahalo wa siku moja juu ya kujikinga na maambikizi mapya ya ukimwi uliofanyika jana shuleni hapo,
Wanafunzi wa shule ya sekondari St Benedictine Hanga wilayani Namtumbo,wakiiangalia chini jana wakati wa mdahalo juu ya masuala ya ugonjwa wa ukimwi ulioendeshwa na idara ya maendeleo ya jamii ya halmshauri ya wilaya ya Namtumbo kupitia mpango wake wa elimu ya ukimwi mashuleni uliofanyika shuleni hapo,
Wanafunzi wa shule ya sekondari St Benedictine Hanga wilayani Namtumbo wakimsikiliza mwezeshaji wa masuala ya ukimwi kutoka idara ya maendeleo ya jamii ya wilaya hiyo Peres Kamugisha hayupo pichani wakati wa mdahalo wa siku moja juu ya namna ya kujiepusha na maambukizi mapya ya ukimwi uliofanyika shuleni hapo jana.PICHA NA MUHIDIN AMRI

No comments:

Post a Comment