WAZIRI wa Ujenzi Dokta John Magufuli ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanamwandikia majina ya wakurugenzi na watendaji wanaotumia fedha za barabara katika kulipana posho na wale wanaokaa nazo bila kuzifanyia kazi ili apeleke kwa Rais na kuhakikisha wanafukuzwa kazi ikiwemo chato na longido.
Magufuli alitoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam katika ufunguzi wa kituo cha mabasi Mbezi mwisho wilaya ya kinondoni ambapo alisema kuwa serikali imekuwa ikitenga fedha kwa halmashauri lakini watendaji wake wamekuwa wakizitumia kwa shuguli nyingine.
Aliiagiza Tanroad akisema “Nyie Tanroads nawapa siku tano muhakikishe hakuna gereji bubu yoyote ,nyumba wala wafanyabiashara walioingia katika hifadhi za barabara wanaondoka hata kama bendera ya CCM imewekwa barabarani ondoeni lazima kufika mahali sheria ifanyiwe kazi lasivyo msongamano hautaisha na katika hili swala siasa liwekwe pembeni” alisema Magufuli.
Magufuli pia alitoa agizo la kuhakikisha ujenzi wa choo,uzio na ofisi katika kituo hicho unamalizika mapema na kuipa Tanroads mamlaka ya kukisimamia kituo hicho ikiwemo daladala zote kutolipishwa.
Aidha alitumia fursa hiyo kupandisha hadhi baadhi ya barabara kujengwa kiwango cha lami ikiwemo ya barabara ya Malamba mawili mpaka tabata na ya mbezi mpaka Tegeta.
Aidha aliwataka wananchi kuhakikisha wanatunza kituo cha mbezi na vinginevyo ikiwa ni pamoja na kutokutupa uchafu katika mitaro na kutovamia hifadhi za barabara kwa kujifanya hawajui sheria kwani huo si utetezi.
No comments:
Post a Comment