Ile sherehe kabambe ya wanafunzi wote waliomaliza shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim miaka ya nyuma, imeahirishwa hadi Jumamosi ya Juni 30, 2012 katika ukumbi utakaotangazwa baadaye. Mabadiliko haya ni kuitikia maombi na kutoa nafasi kwa wenzetu wengi walio mikoani na nje ya nchi ili waweze kushiriki kikamilifu katika sherehe hii hiyo.
Lengo kuu la mkusanyiko huo ni kukutana, kufahamiana, kujua nani yuko wapi na anafanya nini ili hatimaye tuweze kuunda mtandao na kuendeleza mema yaliyopo.
Kamati maalum ya muda ya kuratibu mkusanyiko huo pamoja na kuangalia taratibu nyingine imeshaundwa. Vikao vya wadau vyenye kulenga kufahamiana, kuandikishana majina ya wanaopenda kushiriki na kupanga mikakati ya kufanikisha tukio hili, inafanyika kila Ijumaa kuanzia saa 11:00 hadi saa 1:00 jioni, katika ukumbi wa New Happy Hotel - juu ghorofani, iliyopo mtaa wa Ungoni na Kipande, jirani na zamani mgahawa wa Chef's Pride, maeneo ya Lumumba, Kariakoo hapa jijini Dar Es Salaam. Karibuni sana tukumbukane na tufahamieni zaidi.
Ukisikia au kusoma taarifa hii unaombwa uwaarifu na wengine.
Kwa mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana na kamati ya muda kupitia:
Bi. Mambo Tambaza (0713236110) Mwenyekiti
Bw. Abou Liongo (0762298087) Mjumbe
Cast Vumi 0756 232821, 0713 232821(Mjumbe)
Abbas Mbonga 0767606970 (Mjumbe)
Barua pepe: kinondonireunion@gmail.com
USIKOSE NAFASI YA PEKEE YA KUKUMBUKANA NA KUFAHAMIANA
No comments:
Post a Comment