Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akikung'guta gitaa la solo leo leo alipopata fursa ya kipekee kujiunga na Bendi ya Twanga Pepeta "Kisima Cha Buruduni" na kufanya nao mazoezi ndani ya ofisi za Aset. Baada ya kufanya makamuzi ya nguvu ilidhihirika wazi kwamba ukiachilia mbali siasa Nape ni msanii mkali wa kuimba, na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki. Aidha Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka alifurahishwa na kumshukuru sana Nape kuja kuwatembelea na kuwapa sapoti, vilevile alimuahidi kuwa nafasi yake itakua wazi kwenye bendi mara tu atakapo amua kuachia ngazi kutoka katika jukwaa la siasa na kuamua kujiunga katika tasnia ya muziki.
Nape akipapasa Kinanda
![]() |
Asha Baraka akimfurahia Nape wakati akifanya vitu vyake |
Kija akimwangalia kwa makini Nape akipiga gitaa la Bass
Nape Nnauye akipiga Drums huku Msafiri Diouf akiimba
No comments:
Post a Comment