Mazoezi ya kucheza yakieendelea kutoka kwa Dansa wa Twanga Pepeta Mandela alievaa t shirt ya kijani.
Baada ya kumaliza mchakato wa usajili na usaili wa kutafuta vipaji vipya ndani ya Music Academy Tanzania hatua iliyofuatia ni kuanza rasmi mazoezi ya nguvu yatakayoweza kuwaandaa na kuwanoa vyema wana academia hao ambao wamefaulu kupita katika mchujo wa kwanza chini ya usimamizi kutoka kwa gwiji na nguli wa Muziki Tanzania Mzee Kalala, ASET na URBAN PULSE CREATIVE. Pia kwa upande wa kucheza dansa mkali kutoka Twanga Pepeta Mandela atakua akitoa mafunzo katika fani hiyo.
Lengo la kuanzisha Music Academy hii ni kufundisha na kutafuta vipaji vipya katika tasnia ya muziki ikiwepo kucheza, kuimba, kutunga, kurap, kupiga vyombo mbalimbali n.k na kutoa fursa ya kujiunga katika bendi, vikundi au kuanza kama solo career/ artist mara tu wanapofuzu ili kuimarisha mziki wa kitanzania na pia kuwapa vijana ajira. Mazoezi hayo yatakuwa yakifanyika mara tatu kila wiki kwa wiki kadhaa ndani ya ukumbi wa Baobab Kinondoni Vijana.
wana academia wakiimba wimbo walioutunga wenyewe.
Mzee Hamza Kalala akiwapa somo la muziki wana academia.
No comments:
Post a Comment