Sunday, March 11, 2012

MICHUZI BLOG EXCLUSIVE: DROGBA AANDAA MNUSO WA HARAMBEE KUSAIDIA UJENZI WA HOSPITALI IVORY COAST

 MSHAMBULIAJI NYOTA WA CHELSEA DIDIER DROGBA AKIONGEA  USIKU WA KUAMKIA LEO WAKATI WA MNUSO WA HARAMBEE YA TAASISI YAKE YA THE DIDIER DROGBA FOUNDATION ALIYOIANZISHA MWAKA  2007 BAADA YA KUGUNDUA KUWA NCHI YAKE INA TATIZO KWENYE SEKTA  YA AFYA NA AKAHIDI KUJENGA HSOPITAL, ILA  KUTOKANA NA VITA VYA MWAKA JUZI KUHUSU MARAISI WALE WAWILI IKABIDI  DIDIER ASUBIRI VITA VIISHE AENDELEE NA JUHUDI ZAKE ZA KUJENGA HOSPITAL.

MWAKA JUZI ALIWEZA KUPATA PAUNDI LAKI NANE NA JANA USIKU ALIWEZA KUPATA ZAIDI YA PAUNI  MILLION  MOJA BAADA YA MNADA WA VITU MBALI MBALI IKIWEMO HOLIDAY YA KUJA TANZANIA ILIYOWEZESHWA NA KAMPUNI YA ONE-PLUS CHINI YA UONGOZI WAKE FINA MANGO. LIKIZO HIO YA SIKU 7 ZANZIBAR ILIWEZA KUNUNULIWA KWA PAUNDI 6500.  UJENZI WA HOSPITALI UNAANZA MARA MOJA KWA KUWA SASA MAMBO NI MSWANO NCHINI  IVORYCOAST. 

DIDIER PIA  ALIFANYIWA SURPRISE MAANA LEO HII ANA CELEBRATE BESDEI YA KUZALIWA KWAKE  NA PIA ALIWEZA KU CELEBRATE GOLI LAKE LA 100 KATIKA LIGI KUU JUMAMOSI. NI MWAFRIKA PEKEE ALIEWEZA KUFIKISHA GOLI LA 100 KWENYE PREMIER LIGI.


MNUISO HUO ULIANZA SAA 1 USIKU NA SAA MBILI KULIKUA NI CHAMPAGNE ALAFU CHAKULA CHA USIKU, MNADA UKAPITISHWA WA VITU MBALI MBALI IKIWEMO TRAINING NA DROGBA MWENYEWE ILINYAKULIWA KWA PAUNDI 30 ELFU, WALIOTUMBUIZA NI MUME NA MKE WA MALI AMBAO NI VIPOFU WANAITWA AMADOU NA MARIAM,PAMOJA NA ESTELLE.
 DROGBA AIKONGEA NA MWANAHABARI
 DROGBA AKILA POZI MNA MDAU YASMIN (KULIA) NA RAFIKIYE
 MASTAA KIBAO WAMATUMBI KATIKA WA LIGI KUU  UINGEREZA WALIHUDHURIA
MDAU YASMIN AKILA POZI NA JOHN TERRY KWENYE MNUSO HUO

No comments:

Post a Comment