michuano ya kombe la NSSF kuanza kutimua vumbi jumamosi hii
Meneja wa Uhusiano wa shirika la hifadhi ya jamii NSSF, Eunice Chiume akikabidhi jezi kwa Mwakilishi wa timu ya TBC,Chacha Maginga kwa ajili ya michuano ya kombe la NSSF CUP inayotarajiwa kuanza siku ya Jumamosi kwenye viwanja vya TCC Sigara,Chang'ombe na Chuo Kishiriki cha Elimu Chang'ombe DUCE jijini Dar, hafla hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa JB Belmont Hoteli,Benjamin Mkapa Tower jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa timu ya mabingwa watetezi wa kombe hilo timu ya Jambo Leo maarufu kama "Wagumu Stars" akipokea jezi kutoka kwa Meneja Uhusiano wa NSSF Eunice Chiume kwa ajili ya timu yao
Mwakilishi wa timu ya wanawake ya Netboli kutoka kampuni ya Mwananchi Communication,Kalunde akipokea jezi za timu yao kutoka kwa Meneja Uhusiano wa NSSF,Eunice Chiume.Picha na Full Shangwe.
No comments:
Post a Comment