Sunday, March 4, 2012

MH. NDUGAI AZINDUA ALBAMU YA KWAYA YA HUIMA NA KUWAASA WAUMINI KUSHIRIKI MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Mhe. Naibu Spika, Job Ndugai akikata utepe kuashiria uzinduzi wa albamu ya Injili ya HUIMA. Anaemsaidia ni Askofu Sebastian Kanzese wa Kanisa la FPCT na nyuma ya Naibu Spika ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Shinyanga, Ndugu Maganga.
Mhe.Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akitoa hotuba yake ya uzinduzi wa albamu ya nyimbo za injili za kwaya ya Huduma za Injili Mashuleni (HUIMA) katika ukumbi wa NSSF mkoani Shinyanga. Mhe. Ndugai alikuwa ni mgeni rasmi katika tamasha la kuzindua albamu ya kwaya ya HUIMA na pia kuongoza harambee ya kuchangia mradi wa Huduma za Injili Mashuleni unaoendeshwa na Kanisa la Full Pentecostal Church of Tanzania (FPCT). Katika hotuba yake Mhe. Naibu Spika alihimiza waumini wa dini zote kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato wa Katiba Mpya katika awamu zake zote kama itakavyokuwa ikielekezwa ambapo hivi sasa wametakiwa kutoa maoni ya nani anafaa kuwemo katika Tume ya kuratibu ukusanyaji wa maoni.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwasalimia waumini wa FPCT katika tamasha hilo.
Umati wa waumini wa FPCT Mkoani Shinyanga uliojitokeza katika tamasha hilo lililofanyika katika ukumbi wa NSSF Shinyanga.

No comments:

Post a Comment