Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba (kulia) akiongea na waandishi wa habari juu ya mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake tarehe 19 mwezi huu ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa utafiti na Takwimu Michael Mhando akifuatiwa na Beatus Chijumba ambaye ni Mkurugenzi rasilimali watu na utawala.
Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Eugen Mikongoti akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 ambapo waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Emmanuel Humba na kulia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na uwekezaji Deusdedit Rutazah.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba (kushoto) akiongea jambo na Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko huo Eugen Mikongoti wakati wa mkutano kati yao na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mfuko huo utatimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake tarehe 19 mwezi huu ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika makao makuu ya Bima ya Afya.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba wakati wa mkutano kati yao uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 ambapo waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zitakazofanyika tarehe 19 mwezi huu.Picha na Anna Nkinda - Maelezo.
No comments:
Post a Comment