Salaam Kaka Issa.
naomba mchango huu uunakirishe kwenye blogi yetu hili,na pengine madaktari wetu wakapitia hapa na kuelewa taratibu zilivyo linapokuja suala la madai ya waajiriwa kwa mwajiri sehemu yeyote ile hapa ulimwenguni.
Kaka Issa,katika kutoa mchango wangu hapa kama mtaalam wa mambo ya utumishi na utawala,sitaegemea upande wowote ule uwe wa serikali ama wa madaktari.
Kwanza naomba madaktari wetu wafahamu kwamba palipo na mwajiriwa kuna mwajiri bila kujali kama ujira unaolipwa kama fidia ya kazi aliyoifanya mwajiriwa unalipwa kwa masaa(hourly pay wage) ama kwa mwezi(monthly base pay).
Kwa mantiki hiyo hapo juu ni wazi kwamba kila mwajiriwa anapokubali ajira au anapokubaliwa na mwajiriwa kuwa maombi yake ya kazi yamekubaliwa ni lazima asaini mkataba wa ajira bila kujali kama ni kibarua(cheap labour) ama mwajiriwa chini ya masharti ya kudumu(permanent terms employment)
Nanacho taka kukizungumzia hapa ni makubaliano na masharti ya mkataba unless mkataba uwe haujakidhi kiwango chini ya Labour Laws and Employee Relations ya nchi husika.
Katika sheria hii kuna mambo mawili yaliyoanishwa ama kuelezwa bayana juu ya nini na kipi kifanyike kwenye terms na conditions za ajira baina ya mwajiriwa na mwajiri.
Mambo haya mawili yanagusa na kulenga benefits mbalimbali ambazo ni haki ya mwajiriwa kuzipata kutoka kwa mwajiri wake bila kujali kama masharti ya ajira ni ya labour pay bases ama permanent pay bases.
Mambo haya mawili ni :
1.Faida,ujira ama (fidia)zinazostahili kutolewa kwa mwajiriwa kisheria(legally required benefits) na mwajiri.Zaweza kuwa pesa ama huduma.
Hizi zinashirikisha benefits zote chini ya sheria ya Social Security Fund Act ya Tanzania(1997),Workers compensation Act ya (2008), na Family and leave Act(hapa kwetu vifungu vyake vipo kwenye sheria ya Employment and Labour Relations Act ya 2004.Katika mfumo wa ajira ndani ya nchi yetu benefts zote zilizo chini ya sheria hizo 3 ni za lazima kisheria kutolewa na kutekelezwa na mwajiri kwa mwajiriwa.
Pasipo kufanya hivyo mwajiriwa kupitia vyama vya waajiriwa (Trade unions) wanaweza kumshitaki mwajiri kwenye Mahakama ya Kazi ama Tribunal yeyote inayo husika na usuruhishaji wa migogoro baina ya hizi pande mbili ama sivyo kuanzisha migomo hili kumshinikiza mwajiri,atimize kile kinachodaiwa na waajiriwa au madai yao kwa ujumla ya kipengele hiki.
2.Faida,ujira ama fidia zinazotolewa kwa mwajiriwa kama kipenda roho cha mwajiri(Discretionary Core Fringe Benefits)Hizi ni fidia ama ujira unaotolewa kwa mwajiriwa kama kipenda roho tu cha mwajiri, kumfanya mwajiriwa ajisikie vizuri kiroho,kumuongezea motisha ama kumfanya akabiliane na ugumu wa gharama za maisha.
Hizi zinashirikisha: program za kumlinda mtumishi kama matibabu,anapokoswa ajira,kutojiweza,ulemavu,ajali nk.
Malipo ama ujira wa kutokufanya kazi-Paid Time Off ambao mwajiriwa hulipwa anapokwenda mapumziko,likizo ya ugonjwa ama masomoni nk.
Huduma-hizi ni huduma anazozipata mwajiriwa kama kupata msaada wa chakula cha mchana na familia yake kutoka kwa mwajiri,usafiri(kupewa gari ama pikipiki,huduma za kushiriki mashindano ama michezo mbalimbali ya kumfanya mtumishi awe safi kimwili na kimawazo.
Kaka Issa nimeeleza vya kutosha juu ya mahusiano yaliyopo na yanayotakiwa kuwepo juu ya fidia anazostahili mwajiriwa kutoka kwa mwajiri wake.
Hoja yangu ni ipi kwa kuhusisha mgomo wa madaktari wetu?
(A)Naomba madktari wajue na kutambua kuwa kuna fidia ama stahili wanazopewa kutokana na kipenda roho cha mwajiri.(Discretionary Benefits).
(B)Naomba madaktari wetu watambue pia kuwa kuna fidia ama ujira wanaopaswa kupata kisheria bila kujari mwajiri ni serikali ama mtu binafsi.Kama kuna fidia ama ujira niliouainisha hapo juu wa kisheria na madaktari ama mwajiriwa yeyote haupati,anzeni sasa kuufatilia.
(C)Pamoja na kuwa mtaalamu wa mambo ya utumishi na utawala,hakuna sehemu yeyote niliyoelekwezwa ama kujiridhisha kwa kusoma kuwa,mwajiriwa ana mamlaka ya kisheria kumlazimisha mwajiri wake kumfuta kazi,kumfukuza kazi ama kumsimamisha mwajiriwa mwenzie kwa sababu hatendi majukumu yake vizuri kama wanavyo dai madaktari wetu.
(D)Nawaomba madaktari wetu wapitie madai yao ya mwanzo upya hili wajiridhishe wazi kwamba ni mambo yapi wanapaswa kuyasimamia kudai haki na madai yao ya kisheria.
Sheria ya kazi na mahusiano kazini ina mipaka yake linapokuja suala la madai ya mwajiriwa.
Hitimisho.
I:Nawaomba waaajiriwa watambue haki zao hizi katika makundi niliyo yaainisha hapo juu.
II:Nawaomba madaktari wadai madai yao ambayo wanapaswa kupewa kisheria bila kuathili upande wa pili wa wananchi wanaohitaji huduma zao za kitabibu.
III:Nawaomba madaktari wasiendelee kuishinikiza serikali (mwajiri)kuwafukuza kazi ama kuwasimamisha waajiriwa wenzao.Mh.Waziri na Naibu Waziri.
IV.Naiomba serikali itimize ahadi zake zote ilizotoa kwa waajiriwa wake ikiwa ni pamoja na kuwaboreshea zile discretionary benefits.
"Kila jambo linawezekena ila approach inaweza kufanya lisiwezekane"
Joachim K.Global
No comments:
Post a Comment