Baadhi ya wananchi wa Kata ya Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro wakiangalia maji yaliyojaa kwenye mto Mkundi na kusambaa kwenye mashamba ya wakulima wa Tarafa ya Magole, kama walivyokutwa darajani hapo na mpiga picha wetu.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Adam Malima ( kulia) akijadiliana na msajiliamali,Adam Masemo,( aliyenyoosha mikono miwili mbele ) anayefanya biashara ya kuuza mafuta ya petroli kwenye chupa za plastiki kwa madereva wa Pikipiki ‘ Bodaboda’ eneo la Magubike, Wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro.
Mkulima wa Kata ya Dumila, Tarafa ya Magole, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, Mariam Kisongela, akitoka shambani kwake baada ya kuona maji yamezingira mashamba yao wakati wakiwa mashambani,kama alivyokutwa eneo hilo.Picha zote na John Nditi
No comments:
Post a Comment