Thursday, March 15, 2012

MAONI YA MDAU KUHUSU LIBENEKE LA MASUMBWI YA WACHEZAJI WA YANGA UWANJANI

Uncle samahani , kwanza pole na pia pongezi nyingi kwa kuuunganisha Uma .
Nimetazama Video ya Young Africa na Azam na kuachwa na Majonzi makubwa . Amini usiamini nilishindwa hata kupata usingizi . Ningefurahi sana kama jambo hili wadau tungelijadili kwa kina haswa kwa sisi wadau wa soka.

Swala hili ni Doa kwetu na aibu kubwa kwa nchi Yetu vile vile kwa Wana Young Africa damu ulimwenguni kote . Hawa ma bwana wadoogo hawafahamu kuwa wao ni mabalozi wa mamilioni ya Wana Yanga Ulimwenguni . vile vile ni vioo vya watoto wanaochipukia , sasa kama baba anakojoa kitandani , mtoto naye afanye nini ?

Bila kukimbilia kutupia lawama kwa TFF au Polisi , kwanza ni kwa hao wachezaji waliotuchafulia jina wana Young Africa , enzi zile kuichezea yanga ni fahari kubwa hata kama haupati kitu haswa ..
Ndio Maana hata Africa Nation Cup inabidi tuchague Timu ya kushangilia ,Tazama majirani zetu Zambia , Kongo - TP Mazembe , siye tunaishia kufanya ujinga tu .

Tafadhali Mjomba tubandikie kibao cha gwiji PEPE KALE.... " Young Africa `` ,angalau kitupoze Roho , enzi zile Yanga ikicheza mtoto hatumwi dukani . Haya mambo ya masumbwi walikua nayo Simba sio sie.

Inapaswa wachezaji wetu wa sasa kupata elimu ya kujielewa pia , jambo kama hilo lingetokea simba na yanga , mashabiki si tungekamatana pia ? yale yale ya Misri ? , Mchezaji Huwezi tu kukurupuka kama kichaa na kufanya ujinga wako kiwanjani , alafu bado unataka kucheza professional Ulaya , Mnawachafua majina ya watanzaia wachache wanajaribu kivyao ughaibuni .

mbona mkipelekwa ulingoni kamasi zinawatoka .
Roho inauma.
Mdau .

No comments:

Post a Comment