Thursday, March 15, 2012

Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Zanzibar

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Abdalla Mwinyi akitoa hotuba katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar  katika Ukumbi wa Eacrotanal mjini Zanzibar. Kushoto yake ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo wa Zanzibar Bihindi Hamadi Khamis na kulia kwake ni Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA)Sudi Mohd Masoud
Wanafunzi kutoka katika Skuli ya Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja wakitoa burudani katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar 
 Mwanafunzi kutoka skuli ya Vikokotoni Machano Bakari Hussen akipokea zawadi na Kumshukuru Mungu baada ya Kushinda katika chemsha Bongo ya Maswali ya papo kwa papo huko katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar .Picha na Yussuf Simai Ali-Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment