Saturday, March 10, 2012

kituo cha kukuza na kulea watoto wenye vipaji vya michezo chafunguliwa mjini songea

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu mkoani Ruvuma (FARU) ambaye pia ni mkurugenzi wa bodi ya kituo cha michezo cha Good hope sport center,Joseph Mapunda akizungumza wakati wa kikao cha kutambulisha mpango mzima wa kituo hicho kwa wadau wa michgezo mkoani humo jana,kulia ni mshauri wa michezo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw Hassan Katuli.
Kaimu katibu tawala msaidizi utawala wa mkoa wa ruvuma Gharib Lingo,akizungumza na wadau wa michezo wa mkoa wa Ruvuma (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kituo cha kukuza na kulea watoto wenye vipaji vya michezo kutoka sehemu mbalimbali za mkoa huo cha Good Hope sport center kilichoanzishwa na mwamuzi mstaafu wa mpira wa miguu hapa nchini Bw Joseph Mapunda wa pili kulia aliyekaa mjini songea.
Mkuu wa kituo cha michezo kanda ya kusini Vicent Nmanda Mbaya akitoa nasaha kwa wadau wa michezo wa mkoa wa Ruvuma wakati wa ufunguzi wa kituo cha kukuza vipani na kulea watoto cha good hope sport center mjini songea,kulia ni kaimu katibu tawala msaidizi utawala kutoka sekretalieti ya mkoa wa Ruvuma Ghalib Lingo na kulia ni mkurugenzi wa kituo hicho Joseph Mapunda.PICHA NA MUHIDIN AMRI.

No comments:

Post a Comment