Hilo banda la ghorofa hapa kwetu Zenj tunaita (roshani) limeshazeeka na liko hali mbaya, wakati wa upepo hayo makuti, mbao zilizotumika kulijengea na mambati hupeperuka na kuangua chini, hebu fikiria watoto na wenye nyumba hiyo hapo jirani,watakuwa wapo katika hali gani, mama mkaazi wa mtaa huu wa Bwejuu umangani lilipo banda hili anasema hana amani hata kidogo na hali hii iliyosababishwa na wenye chao wako wapi viongozi au tunasubiri hadi liangukie hii nyumba tuje kuwalaumu kikosi cha uonokozi wamechelewa kuja kuokoa majeruhi??????
huu ni ufukwe wa bahari nzuri ya Bwejuu lakini sasa si ufukwe tena bali ni jalala lenye uvundo na harufu mbaya, wananchi wanapaswa wasitupe taka hapa na badala yake wawekewe jalala la kutupia taka ili ufukwe ulete haiba yake.
No comments:
Post a Comment