Wednesday, March 14, 2012

jinsi mwamuzi israel mkongo alivyopigwa na wachezaji wa yanga

Mwamuzi Israel Mkongo akipigwa na wachezaji wa Yanga  kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliokutanisha timu hiyo  ya Jangwani na timu ya Azam FC kutoka Chamazi ambapo Yanga ilikandamizwa magoli 3-1 na wauza Sembe hao wa Chamazi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Mwanzo ulikuwa ni mchezo mzuri uliokuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande lakini mambo yalibadilika mara baada ya Azam kuandika goli la kwanza, mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga alionekana kumlalamikia refa mara kwa mara jambo ambalo refa alimuonya mara kadhaa lakini, hata hivyo Niyonzima aliendelea baada ya muda, alitolewa nje kwa kadi nyekundu, jambo ambalo lilizua tafrani uwanjani huku makonde yakirushwa hovyo, baadae naye mchezaji Nadir Haroub Canavaro alipewa kadi nyekundu kutokana na vurugu hizo na kuzua tifu lingine uwanjani.

No comments:

Post a Comment