Napenda kutoa mchango wa mawazo kwa watanzania wenzangu kuhusu kusaidia uchumi wetu kufuatia ugumu wa maisha, hasa siku za karibuni, unaosababishwa na kuyumba kwa uchumi katika nchi zilizoendelea, ambazo ndizo mama mlishi wa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania. Kuwepo kwa ugumu wa maisha kisiwe ni kikwazo pekee cha kushindwa kujikwamua kimaisha. Matatizo yetu mengi ya kiuchumi, na hata ya kijamii, hayatapata ufumbuzi toka kwenye vitabu tunavyosoma vyuoni au mashuleni kwani hata silabasi yetu ya elimu haiyatambui. Tukiyafanyia kazi yaliyotajwa hapo chini, nina imani maisha ya mtanzania wa kawaida yatainuka na hivyo kuongeza maendeleo ya haki nchini.
1. Watanzania tulipe kodi- Sehemu kubwa ya uchumi wetu imeshikiliwa na 'black market' pamoja na umachinga. Sehemu hizi hazijatengenezewa mazingira mazuri ya kuwezesha kujituma kulipa kodi ya mapato.
2. Watanzania tuwe wabunifu- Tuangalie nyuma nasi tuanze kusafirisha ubunifu wetu nje ya nchi sawa na wenzetu wachina wanavyofanya hivi sasa. Inakuwaje tunajisifia kunywa 'Heineken' ambayo inaua soko la rubisi, kimpumu, machicha n.k
3. Watanzania tusikubali kutoa rushwa- Tunapotoa rushwa hatusaidiwi bali tunaibiwa haki yetu ya kuhudumiwa, rushwa sio Tip!
4. Tusichukue mikopo- Kuna ukweli kwamba uchina, India na Vietnam zinaendelea kwa kasi tokana na wananchi wake kujijengea rasilimali wenyewe. Mikopo inarudisha nyuma maendeleo; inajenga tabia 'Tegemezi'- sababu kubwa iliyorudisha maendeleo ya bara la Afrika.
Salaam
Jogoo Makunja.
No comments:
Post a Comment