Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa kambi rasmi bungeni,Mh. Freeman Mbowe (wa pili kulia) akijadiliana jambo na Wadau wa chama hicho waliopo mjini Arumeru muda mfupi baada ya kuwasili eneo hilo tayari kwa uzinduzi wa Kampeni ya Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki leo ambapo Mh. Mbowe atatumia fursa hiyo kulihutubia Taifa juu ya Mustakabali mzima wa nchi yetu.
Mgombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA),Joshua Nassari akiwa na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Arusha,Mh. Joyce Mukya (CHADEMA) wakitafakari mawili matatu kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa kampeni leo.
Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Yohana Natse akiwasili kwenye uwanjani hapo tayari kwa uzinduzi wa kampeni za Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki leo.
Mkurugenzi wa ulinzi na usalalma taifa, Ndg. Wilfred Lwakatare akiweka mikakati sawa.
No comments:
Post a Comment