Sunday, March 4, 2012

Ajali ya lori junction ya kwenda Wazo Hill Tegeta

Habari Ankal,

Leo maeneo ya Tegeta katika Junction ya kwenda Kiwanda cha cement cha Twiga (wazo Hill), imetokea ajali ambayo imeihusisha lori lilibeba kifusi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya new bagamoyo. Lori hilo lilikuwa linatokea maeneo ya kiwanda cha cement cha Twiga likiwa limejaza kifusi.

Wakati linashuka kuelekea junction ya bagamoyo road, break zikakatika. kilichotokea ni lori kumgonga mtu mmoja ambaye alifariki papo hapo, halafu likaruka barabara na kwenda kuigonga pick up iliyokuwa imepaki pembeni na almanusra iingie katika duka.

Kutoka kwa mdau wa Tegeta.

No comments:

Post a Comment