Sunday, March 11, 2012

yale yaleeeeeee,,,,,,mti waziba njia ya kaole, bagamoyo, hakuna wa kuuondoa

Ankal, habari za kazi, hongera kwa kazi nzuri ya kuiabarisha jamii mambo muhimu yanayowahusu.

Nipo Bagamoyo kwa sasa kama mtalii wa ndani, kama ijulikanavyo Mji huu ni maharufu kwa kuwa na vivutio mbali mbali vinavyo wavutia wengi kutoka nje na ndani ya nchi kuutembelea mji huu.

Kaole ni moja ya sehemu muhimu sana kwa utalii, njia ya kwenda Kaole kutoka mjini Bagamoyo inapitia Chuo cha sanaa, lakini kwa sasa njia hiyo imefungwa baada ya mti kuanguka katikati  ya Barabara hivyo kuwazuia  waendao kwa magari, hali inayo sababisa kero kubwa sana kwa watalii. Napenda kujiuliza hivi uongozi wa Halmashauri upo wapi? Inachukuwa muda gani na shilingi ngapi kuutoa mti huo ili kulinda hesha ya mji wa Bagamoyo? Naushari uongozi wa bagamo uchukuwe hatua za haraka za kuuondoa mti huo, Kwanza hata kiusalama unapunguza kasi ya kazi hiyo maana umezuia mawasaliano kati ya Kituo cha Polini na Mji wa Bagamoyo.

Hasanteni.
Mdau Sixmund

No comments:

Post a Comment