Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,Inaeleza kuwa Boss wa zamani wa TBC (Tanzania Broadcasting),Tido Mhando (pichani) amekuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Uchapishaji wa Magazeti ya kila siku hapa nchini ya Mwananchi Communication Limited,kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mkurugenzi Mtendaji wa Zamani wa Kampuni hiyo,Sam Shollei.
Globu ya Jamii inatoa pongezi kwa Bw. Tido Mhando kwa kupata nafasi hiyo na kumtakia kila la kheri katika utendaji wa kazi yake hiyo mpya.
No comments:
Post a Comment