Tuesday, March 20, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AFUNGA MAFUNZO YA WAJASIRIAMALI WA UFUNDI YALIYOENDESHWA NA SIDO.

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi Sido mkoa wa Rukwa, sambamba na wajasiliamali wapatao 55 walioshiriki mafunzo ya ujasiliamali katika fani tofauti na kufanyika katika mji wa Matai.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akikabidhi Cherehani kwa Zaituni Matofali ambaye ni miongoni mwa washiriki 55 wa mafunzo hayo ambao walipatiwa vifaa mbalimbali vya ufundi na SIDO kwa ushirikiano na Shirika lisilo la Kiserikali kutoka Uingereza liitwalo Tools for Self Reliance. Wa kwanza kushoto Mtaalamu wa Ufundi wa Mafunzo hayo na wa pili Meneja wa Sido Mkoa wa Rukwa Martin Chang'a.
Mkuu wa Mkoa akikabidhi Mashine ya Kuchomelea (Welding Mashine) kwa Charles Msangawale muda mfupi kabla ya kufunga mafunzo hayo. Vifaa mbalimbali vilikabidhiwa kwa wajasiriamali hao vikiwa na thamani ya Shilingi Millioni 37.5 Tshs. Mkuu huyo wa Mkoa alisema vifaa hivyo vikitumika vizuri kwa lengo lililokusudiwa basi vitaongeza Ajira na kipato kwa wajasiriamali hao na wengine watakaonufaika kupitia vifaa hivyo.Habari zaidi ingia hapa

No comments:

Post a Comment