Saturday, March 10, 2012

msiba dar es salaam na karagwe

 KANALI ADOLF PETER MUTTA WA MAKAO MAKUU YA JWTZ ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABA YAKE MZAZI MZEE PETER  LUGALABAMU (PICHANI)  KILICHOTOKEA JUMAMOSI TAREHE 10/03/2012 KATIKA HOSPITALI KUU YA JWTZ  LUGALO JIJINI DAR ES SALAAM. 


MIPANGO YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU KWENDA KARAGWE MKOANI KAGERA INAFANYIKA NYUMBANI KWA KANALI MUTTA LUGALO DAR ES SALAAM. 

MWILI WA MAREHEMU UTASAFIRISHWA JUMATATU TAREHE 12/03/2012  NA KUZIKWA JUMATANO TAREHE  14/03/2012 NYUMBANI KWA MAREHEMU HUKO KARAGWE,  KAGERA.  

HABARI ZIWAFIKIE WANAUKOO WOTE WA ABAHINDA WA KAMACHUMU, UKOO WA KAMUNIGA, UKOO WA  BIITA, FAMILIA YA MZEE KINANILA, FAMILIA YA HELMAN WA KAMACHUMU, NDUGU WOTE NA MARAFIKI.

No comments:

Post a Comment