ANKAL SALAMALEKO...
NIMERUDI TENA MKUU, SAFARI HII NNA SWALA NATAKA UFAFANUZI WA WADAU WAKO LUKUKI WA LIBENEKE.
SWALA LANGU NI KUHUSU HII MITANDAO YA JAMII (SOCIAL NETWORKS) AMBAYO KWA KWELI IMELETA MABADILIKO MNO KATIKA JAMII - IMEANGUSHA SERIKALI (TUNISIA, MISRI NA LIBYA) NA IMEWEZA HATA KUMPELEKA MTU IKULU (OBAMA), KWA HILO NAIPONGEZA.
SWALA SASA JE NINI KINAFUATA (WHAT NEXT)???
NAHOJI HIVYO SABABU HADI DAKIKA HII SIJAONA MITAMDAO IKILETA MAGEUZI CHANYA (POSITIVE) KATIKA HII JAMIII YETU. SANA SANA IMEKUWA KAMA IMEKUJA KUKOSOA NA KJULETA UJUAJI WA KILA KITU, KWA KUWA TU MTU ANAFUNGUA KOMPYUTA YAKE NA KUMWAGA LAZI. LAKINI UKICHUNGUZA UTAKUTA HAKUNA TIJA KABISA KATIKA HII MITANDAO.
WADAU WA LIBENEKE HILI NAOMBA TUJADILI. NI KWELI KWAMBA MITANDAO YA KIJAMII INA UWEZO WA KUJENGA/KUBOMOA LAKINI HAINA UWEZO WA KULETA MABADILIKO MBADALA WA HAYO WANAYOYASHUPALIA???
NAWASILISHA
MDAU SALAMA LEKO
No comments:
Post a Comment