Monday, March 12, 2012

UFAFANUZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI KUHUSIANA NA “KILIO CHA WATANZANIA UGIRIKI”

Kuna Mdau wa ugiriki aliandika 12/03/2012 ‘Kilio cha watanzania ugiriki” na kulikuwa na maoni tofauti yasiyopungua 25.

Kwanza kabla ya yote kichwa chake cha habari kingependeza kiwe “KILIO CHA MTANZANIA” na siyo “KILIO CHA WATANZANIA”

Pili ,kwa kuwa  mtandao umeleta usawa wa mtu au watu kueleza chochote wakitakacho,imekuwa ni ada kwa baadhi ya watu kuelezea   fikra zao kwa kutumia ANONYMOYS  na wengine wakidai wapo nchi fulani kumbe hawapo kabisa katika nchi hiyo.

Mimi niandikae maelezo haya naitwa KAYU LIGOPORA mkaazi wa Athens  ni Katibu wa Jumuiya ya watanzania tuliopo hapa. Napatikana kirahisi kwa email tanzathens@yahoo.com.
Nimelazimika kuuandika ufafanuzi huu baada ya kuombwa na watanzania wengi wanaoishi hapa waliosoma “KILIO CHA WATANZANIA UGIRIKI”
  Ni kweli kuna hali ngumu  ya  kiuchumi ugiriki ukilinganisha na ilivyokuwa zamani.Yeyote ataepinga  hali hili hatokuwa mkweli wa maelezo(Na huu ni ukweli pekee katika maelezo ya  kilio cha Mdau wa Ugiriki).Isipokuwa mdau aliyeelezea kilio chake ametumia maelezo mengi yasiyokuwa na ukweli ili  aweze kuwakinaisha wasomaji wakubaliane na hoja zake.
Kwa mfano 

Anadai kuna majina ya  wageni zaidi ya milioni waliojiandikisha kurudi (akiwemo na yeye) .. Hakuna ukweli wa idadi hiyo kulingana na takwimu za idara husika za hapa.

2.   Anadai pa kulala wanashindwa kulipa hadi kuna wengine wanajipeleka hospitali ili walazwe wapate pa kulala!!!! Namnukuu “Imebidi baadhi yetu kuna ambao wamejipatisha vitanda hospitalini ili kuweza angalau kupata sehemu ya kuweka ubavu na chakula”…Hapa sina comment nawaachia wasomaji, ila tu nchi hii huwezi KUJIPATISHA KITANDA  HOSPITALI KAMA HUUMWI na hasa ukiwa mgeni!!!

  Inakuwa vigumu mno kuwakinaisha wasomaji wenye busara zao kwamba watanzania wa ugiriki kilio chao ni hicho kilichoelezwa na Mdau ANONYMOYS wakati kwamba juzi  juzi watanzania haohao walikuwa wanajirusha na KHADIJA KOPA NA MATONYA na wanajiandaa kumleta mwimbaji mwingine katika kipindi cha Pasaka!!!!

Mwisho,inabidi wanaokuja Ughaibuni  kutafuta maisha waelewe kuwa katika  kutafuta kuna tabu  tofauti ambazo zitawakumba na wanabidi wazivumilie. Ingekuwa maisha ni rahisi kama wanavyodhani basi kila mmoja angekuja Ughaibuni na kurudi Afrika  akiwa milionea.

No comments:

Post a Comment