Katibu Mtendaji wa APRM Bi. Rehema Twalibu akitambulisha ujumbe wa wataalam wanaounda timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM) kwa mhe. Spika. Ujumbe huo ulifika Bungeni leo kukutana na uongozi wa Bunge kwa lengo la kujadili maswala mbalimbali katika utawala bora
Mwenyekiti wa Bodi ya APRM Tanzania Prof Assa Mlawa akitoa neno la utangulizi mara baada ya ujumbe huo kufika kuonana na Mhe Spika Ofisini kwake leo
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akijibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM) mara baada ya ujumbe huo kukutana na uongozi wa Bunge dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni kiongozi wa ujumbe huo Akere Tabeng Muna na kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya APRM Tanzania Prof. Hassa Mlawa
Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM) mara baada ya kukutana nao Ofisi za Bunge Dar es salaam leo. Kulia kwake ni mwenyekiti wa bodi ya APRM Tanzania Prof. Hassa Mlawa na Mhe. Anne Makinda Spika wa Bunge na kushoto ni kaimu katibu wa Bunge Charles Mloka. Ujumbe huo ulifika Bungeni leo kukutana na uongozi wa Bunge kwa lengo la kujadili
Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa kamati za Bunge wakisikiliza kwa makini baadhi ya hoja zilizokuwa zikiulizwa na baadhi ya wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM) ambao walikutana na uongozi wa Bunge leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya fedha za Umma (PAC) Mhe. John Cheyo akijibu baadhi ya maswali kuhusu usimamizi wa Bunge katika maswala ya fedha za umma kwa wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM) ambao walikutana na uongozi wa Bunge leo kujadili masala mbalimbali katika utawala bora
wajumbe wa timu ya kujitathimini katika maswala ya Utawara Bora barani Afrika (Africa Peer Review Mechanism –APRM) wakiwa katika kikao cha pamoja na Spika wa Bunge na wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge mara baada ya kukutana nao Ofisi za Bunge Dar es salaam leo. Picha na Owen David
No comments:
Post a Comment