Saturday, March 17, 2012

Sheria gani ya kiusalama barabarani inapaswa kuchukuliwa kwa madereva wa daladala wa namna hii?

Hapa ni  Kituo cha Daladala Buguruni Sokoni ambapo kuna sehemu nzuri tu ya kuegesha magari haya.lakini kutokana na kutotii sheria ya usalama barabarani,dereva wa gari hii kasimama upande wa barabarani kabisa na upande wa pili wa barabara hii kuna kituo kikubwa cha polisi lakini bado madereva hawa wa daladala hata hawaogopi.
Hapa ni Tabara Matunbi ambapo uzembe wa kusimama na kushusha abiria barabarani unaendelezwa.sasa sijui ni juhudi gani na ni sheria gani za kiusalama barabarani zinapaswa kuchukuliwa ili kulitokomeza kabisa tatizo hili.

No comments:

Post a Comment