Friday, March 16, 2012

Rais Dkt.Kikwete aagana na mabalozi wapya wa Tanzania nchini Italia,Uganda na Msumbiji

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo ameagana na mabalozi wapya watatu watakaoiwakilisha Tanzania nchi za nje.Mabalozi waliokwenda ikulu kumuaga Rais Kikwete ni pamoja na Dkt.James Msekela anayekwenda Italia, Dkt.Ladislaus Komba anayekwenda Uganda na Mhe.Bi.Shamim Nyanduga anayekwenda Msumbiji. Pichani  Rais   Kikwete akizungumza na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Italia Dkt.James Msekela ikulu jijini Dar es Salaam leo
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Uganda,Dkt.Ladislaus Komba ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi Mpya wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Shamim Nyanduga ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu. 

No comments:

Post a Comment