Wananchi wa kijiji cha Shambarai, Kata ya Mbuguni, wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimboni humo leo.
Pamela Sioi akimuombea kura mumewe, mgombea ubunge wa CCM, jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari kwenye kampeni zilizofanyika kijiji cha Shambarai kata ya Mbuguni jimboni humo leo.
Mama Sioi(wapili kulia) akishiriki kuselebuka muziki wa hamasa za Chama, uliporomoshwa katika kijiji cha Msitu wa Mbogo kata ya Mbuguni kabla ya kuanza kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimboni humo leo
"Tupo na ninyi" wanafunzi wa shule ya msingi Msitu wa Mbogo wakisema huku wakionyesha dole gumba msafa wa mgombea ubunge wa CCM Sioi Sumari ulipowasili kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja uliopo jirani na shule hiyo.
Sioi Sumari akiwasalimia wapigakura wake baada ya kumaliza mkutano katika kijiji cha Msitu wa Mbogo
Sioi Sumari akiwaaga wapigakura wake baada ya kumaliza mkutano katika kijiji cha Msitu wa Mbogo, leo.
No comments:
Post a Comment