Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa jana jioni na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Leonidas Gama mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tayari kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Miongoni mwa shughuli ambazo Mheshimiwa Rais atafanya ni pamoja na kuzindua kampeni ya kupinga ukatili na matumizi ya nguvu dhidi ya wanawake ambayo ataizindua kwa kuanzisha safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro iliyopewa jina la “Kilimanjaro Speak Out, Climb Up”.
Shughuli hiyo itakayofanyika kesho Jumatatu, Machi 5, 2012 asubuhi, imepangwa kwenye Lango la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Mbali na kuanzisha kampeni hiyo, Mhe Rais pia atafungua Mkutano wa Mwaka wa Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika kwenye Chuo cha Polisi mjini Moshi.
Hii ni ziara ya kwanza ya Mhe Rais Kikwete katika Mkoa wa Kilimanjaro tokea alipotembelea Mkoa huo wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
kwa mapicha zaidi
No comments:
Post a Comment