Saturday, March 10, 2012

JINSI YA KUTUMIA INTANETI KWA FAIDA

Na Deogratius Kilawe
Dunia sasa ni kijiji hamna namna ya kufanya kuepuka,ni uwanja wa kukabiliana na yote hayo mazuri na mabaya,Nimekutana na mikasa mingi hapa kwetu afrika watu wengi wakitumia intaneti pasipo faida ya kiuchumi au kijamii na kuwaletea majanga ya kupoteza rasilimali muda  pasipo sababu rasmi.

Mara kadhaa imenitokea wakati nikiwa miaka ya mwishoni mwa 1990’s  na mwazoi mwa mwaka 2000’s wakati ndio nilikuwa nipo sekondari nikiingia intaneti café pasipo sababu maalumu,mara  nimefungua tovuti hii,ile na kwa kuwa sikuwa najua tovuti mbalimbali  nikabaki najua google,yahoo,na baadhi tu,lakini kumbe kulikuwa na tovuti muhimu sana ambazo nilikuwa nakosa kupata taarifa nilizokuwa nazihitaji.

Nimeamua kwa moyo mkunjufu kushirikiana na umma  kujua  hili jambo,naamini sio wote lakini ni wengi huingia mitandaoni pasipo au hutaka kupata taarifa lakini kwa sababu ya kukosa taarifa ya tovuti gani nzuri na hivyo kuishia kukosa taarifa muhimu.
UKITAKA MAMBO YA BIASHARA:
MIKUTANO NA USAHILI/INTERVIEW YA ONLINE:
TAARIFA YA HABARI ZA TANZANIA, AFRIKA NA DUNIA
MASWALA YA KIROHO ,HALI YA HEWA , UBINADAMU PAMOJA NA KUJITOLEA
HABARI ZA BURUDANI  DUNIANI NA TANZANIA

KUJUA HABARI ,TAFITI ZA MAMBO NA VITU(MAKTABA YA DUNIA)
PICHA ZA KITAALAMU  NA KUNUNUA PICHA:
MITANDAO YA KIJAMII:
KUNUNUA VITU  MFANO VITABU NK.
MASWALA YA NDOA
Pangilia unachotaka kufanya kwa intaneti,usifanye tu kwa sababu linatokea,kifalsafa tunasema usipopanga  jambo,sio kwamba hujapanga,ila umepanga lolote ambalo litakalo kukuta na likuchuke.Hivyo matumizi ya intanet angalia sana yasiibe sana rasilimali muda yako.

No comments:

Post a Comment