Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango na Fedha ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola, Mhe, Request Muntanga kutoka Zambia ambae pia ni Mweka Hazina wa Chama hicho akiongoza kikao cha Kamati hiyo mjini Lusaka jana, Katika kikao hicho, Sekretarieti ya CPA Barani Afrika ambayo iko katika Bunge la Tanzania iliagizwa kuainisha maeneo muhimu ambayo michango ya wanachama inaweza kuwekezwa nchini Tanzania ili mapendekezo hayo yaweze kupitishwa na Mkutano mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu nchini Afrika Kusini. Kwa hivi sasa fedha hizo za wanachama ziko katika akaunti za chama hicho nchini Tanzania na imeonelewa ni busara kuziwekeza kibiashara ili kuwe na tija zaidi katika kupanua wigo wa mapato ya chama hicho. Kushoto ni Afisa Dawati wa Chama Kamati hiyo, Bi. Elsie Simpamba akifuatiwa na Katibu wa Bunge la Tanzania ambae pia ndio Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dr. Thomas Kashililah. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo kutoka Uganda, Mhe. Elijah Okupa.
Watumishi wa Ofisi ya Bunge ambao pia ni wajumbe wa Sekretarieti ya Chama hicho wakiwa kazini, kutoka kushoto ni Nd. Emmanuel Mpanda, Bi. Amina Magina, Nd. Aubrey Chiwati na Nd. Demetrius Mgalami. Picha na Saidi Yakubu
No comments:
Post a Comment