Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayehusika na Mazingira Mhe. Terezya Hoviza (Mb)akimsikiliza Kaibu Balozi Bw.Justin Seruhere, wakati Waziri huyo na ujumbe wake alipoutembeleza Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, ulipo jijini New York, Marekani.
Mhe. Waziri Hoviza alikuwa hapa kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa kilele ulioandalliwa na Taasisi isiyo Kiserikali ya World Society of Protection of Animals ya Switzland. Mkutano huo ambao uliwashirikisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali duniani ajenda kuu ilikuwa ni Chakula, Lishe na Lilimo Endelevu. Waziri Terezya Hoviza alikuwa mmoja wa wajumbe waliozungumza katika mkutano huo na pia aliongoza moja ya mijadala ya mkutano huo.
Akatumia fursa hiyo kuelezea uzoefu wa Tanzania katika uboreshaji na uendelezaji wa kilimo endelevu na chenye tija, uhifadhi wa chakula na suala zima la lishe. Tanzania ni kati ya nchi chache katika bara la Afrika ambazo zinazalisha chakula cha kutosha na ziada kuunzwa katika nchi za jirani. Mwishoni mwa mkutano huo wajumbe walitoka na azimio ambalo litawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ili mapendekezo yaliyomo katika azimio hilo yaweze kuingizwa kwenye Tamko la Pamoja la Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu maarufu kama RIO +20. Mkutano huo utafanyika mwezi June mwaka huu huko Rio de Janeiro, Brazil.
Mhe Waziri Terezya Hoviza akiwa na Kaimu Balozi, Bw.Justin Seruhere mara baada ya kusaini kitabu na mazungumzo mafupi ambapo Kaimu Balozi alitumia fursa hiyo kuelezea majukumu ya Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Kutoka kushoto ni Katibu wa Waziri, Bw. Joseph Qamara, Mhe. Waziri Terezya Hoviza( Mb) Kaimu Balozi,Bw. Justin Seruhere na Bw. Julius Ningu Mkurugenzi wa Mazingira
No comments:
Post a Comment