Tuesday, March 6, 2012

WAFANYAKAZI WA BENKI YA POSTA WASHEREHEKEA TPB DAY OUT

Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakishindana kukimbiza kuku wakati wa kusherehekea siku yao waliyoiita TPB DAY OUT. Nia ya kuadhimisha siku hiyo ni kuwapa fursa wafanyakazi kukutana na kucheza pamoja nje ya sehemu zao za kazi ili kupumzisha akili na kujenga umoja na upendo kati yao. Wafanyakazi wote walishiriki kucheza michezo mbalimbali kwenye ufukwe wa Kunduchi Beach Resort. Pia walishiriki kwenye mashindano mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa wavu (Volley ball), kukimbiza kuku. Kuogelea pamoja na kucheza muziki.

No comments:

Post a Comment