Saturday, March 17, 2012

SERIKALI YAOMBWA KUHARAKISHA MAFUNZO KWA MADIWANI

Na Mery Ayo,Arusha

SERIKALI imeombwa kuharakisha kutoa mafunzo kwa madiwani wa halmasauri ili yawawezeshe kuwa na uwezo wa kiufanisi katika majukumu yao ya kazi .

Hayo yalisemwa mjini hapa na mwenyekiti wa jumuiya ya tawala za mitaa Tanzania (ALAT) bw Didas Masaburi alipokuwa akiongea katika mkutano wa kujadili changamoto zinazoikabili serikali za mitaa uliofanyika mjni hapa.

Aidha alisema kuwa ili madiwani waweze kuimili majukumu yao ya ila siku ni vema serikali ikaharakisha kutoa mafunzo waliyoaidi kwa kwa madiwai wengi wanashindwakutekeleza majukumu yao kwa wakati muafaka

;ili madiwani waweze kufanya kazi zao kwa makini ni vema serikali nayo ikawawezesha kwa kuwaatia mafunz waliyohaidi kwa muda kwani shughuli nyingi za halimashuri hazifanyiki kwa muda “aisema masaburi

Bw Masburi aliwataka madiwani wote nchini kuhakikisha kuwa wana mshikamano thabiti na kutoa sauti zinazofanana ii kuishinikiza serikali kuwapatia haki zao za msingi.

Akiongelea swala zima la changamoto zinazokabili jumuiya hiyo alsema kuwa ni pamoja nakufutwa kwa ruzuku za fidia zilizokuwa zikitolewa wa serikali za mitaa kufidia kodi zilizofutwa.

Aidha mkutano huo pia utaweza kupokea taarifa ya utafiti uliofanywa na jumuiya hiyo kwenye halimashauri zote hapa nchini ambapo athari hizo ni pamoja na kushindwa kulipia gharama za uendshaji wa halimashauri na mishahara ya watumishi.

No comments:

Post a Comment