Nimetua Bongo kutokea ughaibuni tarehe 3 Machi. Wiki moja baadaye, "laptop" yangu imeibiwa hapa Dar es Salaam, eneo la Sinza.
Ilikuwa ni Apple mpya. Nilikuwa nimeipakia maandishi yangu mengi, miswada na ripoti za utafiti wa kuanzia 1993.Ninachohitaji ni haya maandishi.
Huu ni mchango wa taaluma ambao natoa kwa wa-Tanzania na walimwengu.
Miswada ya vitabu viwili nilitaka kuchapisha hapa Tanzania wakati huu, kwa manufaa ya wanafunzi, walimu, na jamii. Hii "laptop" ukiifungua inakupa jina la Joseph Mbele, na unahitaji "password" ili kuweza kuitumia.
Habari ndio hiyo. Hivi sasa najiona kama mkulima mwenye ari ya kulima, lakini jembe hana. Nakala za miswada ziko ofisini Marekani. Lakini mimi nilipania kufanya kazi kubwa kwa wiki hizi nitakapokuwa hapa Tanzania. Nimekwama
No comments:
Post a Comment