Friday, March 16, 2012

maadhimisho ya wiki ya maji kitaifa yazinduliwa mkoani iringa leo

 Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh.Dkt Christina Ishengoma akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya wiki ya maji mkoani humo yaliyoanza leo kwenye uwanja wa mpira wa Samora,ambapo Idara mbalimbali zimejitokeza kwenye ufunguzi huo,shoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo,Bwa.Aman Mafuru.Maadhimisho hayo yanayofanyika Kitaifa mkoani Iringa yamedhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti,ambapo mwaka huu kampuni hiyo imechangia kiasi cha shilingi milioni 300 kufanikisha maadhimisho hayo.
Shoto ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho hayo,Bwa.Aman Mafuru.akisoma ripoti ya maadhimisho ya Wiki ya maji yanayofanyika Kitaifa mkoani Iringa kwa Mkuu wa Mkoa Mh. Dkt Christina Ishengoma wakiwemo na baadhi ya viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakishuhudia .Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni MAJI KWA USALAMA WA CHAKULA.
Mkuu wa Mkoa Mh. Dkt Christina Ishengoma akisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo viongozi wa mkoa huo waliofika kwenye maadhimisho ya wiki ya maji mapema leo jioni yanayofanyika kwenye uwanja wa Samora.
Mkuu wa Mkoa Mh. Dkt Christina Ishengoma akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bi Teddy Mapunda,ambao ndio wadhamini wa maadhimisho hayo ya wiki ya maji yanayofanyika kwenye uwanja wa Samora.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL),Bi Teddy Mapunda  akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Dk Christina Ishengoma mara alipotembelea kwenye banda la kampuni hiyo,kati ni Meneja huduma za Jamii  (SBL) Nandi Mwiyombela.Picha zaidi Bofya hapa

No comments:

Post a Comment